Ufuska mtupu! Mnenguaji wa kiume wa
Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, Bakari Kisongo ‘Mandela’ ametoa
kali ya kufungia mwaka baada ya kunaswa ‘laivu’ akililia penzi kutoka
kwa dada aliyetajwa kwa jina moja la Zainab.

Bakari Kisongo ‘Mandela’ (kushoto) ametoa kali ya kufungia mwaka baada ya kunaswa ‘laivu’ akililia penzi kutoka kwa dada Zainab.
Tukio hilo la aina yake lililoshuhudiwa
na ‘fotografa’ wetu lilitokea juzi nje ya Ukumbi wa Mango Garden,
Kinondoni jijini Dar ambapo Twanga ilikuwa ikivurumisha burudani ya
Sikukuu ya Krismasi.

Bakari Kisongo ‘Mandela’ (kushoto) akilazimisha penzi
Mara baada ya bendi hiyo kumaliza
kufanya onesho lake majira ya saa 9:30 usiku, mnenguaji huyo alionekana
akizama kwenye Baa ya Uhuru Peak inayotazamana na Mango kisha akamwita
msichana huyo ili waondoke.

Bakari Kisongo ‘Mandela’ (kushoto) kanaswa ‘laivu’ akililia penzi kutoka kwa dada Zainab.
Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa
karibu, kulitokea kama mtafaruku kwani msichana huyo alikataa katakata
kuondoka na mnenguaji huyo.
Baada ya kuona hivyo, Mandela alitumia
mbinu mbadala (nguvu) ambapo alimvutia mrembo huyo ndani ya Bajaj
iliyokuwa imepaki eneo hilo ndipo mtafakuru ukazuka.
Huku na huku, dada huyo alipata upenyo
ambapo alichoropoka na kutoka nje ambapo Mandela naye alimrukia na
kuanza kumlilia huku akilazimisha mambo ya kikubwa hadharani ikiwepo
‘kudendeka’.
Hata hivyo, Mungu mkubwa kwa sababu
mrembo huyo alifanikiwa kumtoka Mandela kisha akadandia Bajaj nyingine
na kuondoka kwa kasi huku akimwacha jamaa na mfadhaiko.
Mashuhuda wa tukio hilo walimponda
Mandela wakidai kuwa huo ni ufuska kwani kitendo alichotaka kufanya si
cha kuigwa katika jamii.
Wanahabari wetu walipomtaiti Mandela
kutaka kujua kulikoni kuomba mambo ya kikubwa hadharani hakuwa na la
kusema zaidi ya kusikitika kumkosakosa mrembo huyo.