Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

Saturday, January 18, 2014

OPERESHENI FICHUA MAOVU NOUMA::..BABY MADAHA ANASWA LIVE BILA CHENGA KWA DAU LA MI...KWELI WASANII WA KIKE WA BONGO WANAJIUZA,kubali kataa!!!ashikwa kiutamu....!check hapa!!

AMA kweli maovu yanazidi kuongezeka, shetani naye mbioni siku zote kunasa waliyo wake, kauli hizo zote ziko sambamba na staa wa sinema za Kibongo na mkali wa muziki wa Kizazi Kipya, Baby Joseph Madaha amenaswa baada kuingia mkenge mtego wa kujiuza, Ijumaa limesheheni.

Kumekuwa na skendo kuwa baadhi ya mastaa wa kike Bongo hujihusisha na biashara ya kujiuza ili kujipatia kipato na kufanya sanaa kuwa kama chambo cha kunasa wanaume.

OFM MZIGONI
Oparesheni Fichua Maovu (OFM) chini ya Global Publishers, mwaka jana ilinasa mastaa wawili kwenye mtego wake, mke wa mtu, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ na Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’.
Mwaka huu, OFM imeanza kazi zake ambapo kwa kuanzia iliamua kumtega Baby Madaha aliyejaa kwenye kumi na nane zake.

Mmoja wa wadau wa OFM alijifanya mfanyabiashara kutoka Mwanza ambaye ni mgeni wa jiji a.k.a Ngosha akijipachika jina la Frank ambapo baadaye katika mazungumzo, Baby Madaha alimbana na kutaka ampatie majina matatu ndipo mwana-OFM Frank (feki) akajipatia jina Frank Michael Lugwisha.

ILIKUWAJE?
Mchezo mzima ulianza Januari 13, mwaka majira ya saa 11:52 jioni kwa kuchati kwenye simu ya kiganjani ambapo Baby Madaha aliingia kichwakichwa bila kujua anachati na ‘sumu’ wa OFM kama ifuatavyo;
Frank/OFM: Mambo vipi Baby Madaha? Nilikuwa naomba tuonane.
Baby Madaha: Kuhusu nini?

Frank/OFM: Niwe mkweli, Madaha nimekupenda, nilipofika hapa Dar ndo nikaona nikutafute.
Baby Madaha: Unampendaje mtu usiyemjua?
Frank/OFM: Jamani nakuonaga magazetini na video zako.
Baby Madaha: Safi, so unataka kuniambia nini ambacho sijakisikia?
 Frank/OFM:  Nataka tu-meet (kukutana) Madaha nimetokea kukupenda sana lakini Alhamisi (jana) narudi mkoani Mwanza.

Baby Madaha: Huwezi ku-manage kuwa na mimi, baki kuwa shabiki wangu tu.
Frank/OFM: N’take radhi Madaha, kwa nini nisiweze, kikubwa kipi?
Baby Madaha: Huh! Tuma vocha tuone how worth are you? (Tuma vocha tuone utajiri wako)
Frank/OFM: Acha utani bwana, vocha kitu gani, ongea mambo makubwa Madaha
Baby Madaha: Hahaha…yote ninayo-except vocha tajiri.

Frank/OFM: Acha bwana. Vocha ndo kikwazo kwako?
Baby Madaha: Yap! Kama hutaki acha au unadhani natumia wireless kuchati na wewe?
Frank/OFM: Madaha wewe ni mkatili kiasi hicho?

MAMBO YASIMAMA KWA MUDA
Masuala ya kuchati yalisimama kwa muda lakini ilipofika saa 2:22 usiku, mazungumzo yaliendelea ambapo siku iliyofuata Frank wa OFM aliamua kuendelea kumtengenezea mtego ili kujiridhisha kama ni kweli baadhi ya mastaa wa Bongo wanafanya biashara hiyo haramu.
Januari 14, mwaka huu, majira ya saa 5:00 asubuhi, Frank wa OFM alianza tena kuchati na Baby Madaha kama ifuatavyo;

Frank/OFM: Mambo Madaha? Mi Frank
(akaamua kumpigia simu Frank wa OFM, ilikuwa mshtuko kwa Frank kwa sababu hakujipanga kuongea naye kwa hiyo hakupokea simu ya Baby Madaha ambayo ilipigwa saa 6: 30 mchana.
Dakika moja baadaye, Baby Madaha alituma meseji ya kumtoa hofu Frank wa OFM;
Baby Madaha: Frank ‘am calling you in vain uh afraiding of me (Frank nakupigia kwa nia njema unaniogopa?)

Frank/OFM: Sorry nilikuwa tight, naweza kupiga?
Baby Madaha: Yap!
Frank/OFM: Frank wa OFM aliongea na Baby Madaha na kuanza kumchomekea ambapo alitoa ushirikiano wa kutosha na kuonesha nia ya kujenga uhusiano huku akimtaka staa huyo kuwa ‘siriaz’ akimuahidi kuwa atakuwa naye na kuwa ajenti wake wa muvi jijini Mwanza.
Baada ya maongezi ya kutongozana kwenye simu, Frank wa OFM alimtumia tena meseji Baby Madaha kama ifuatavyo;


Frank/OFM: Nimefurahi sana kuongea nawe, sijui itakuwaje tukionana?
Baby Madaha: Wait, you I’ll see.
Frank/OFM: Eti ee, nimetokea kukupenda sana.
Baby Madaha: Thanks.

Baada ya hapo Frank wa OFM alimaliza kumtumia ‘sms’ siku hiyo, ilikuwa saa 9:12 alasiri.
Hata hivyo, Frank wa OFM aliamua kumhoji zaidi kupitia sms akitaka kujua hasa akiwa naye hata kwa saa tatu atataka shilingi ngapi?
Frank/OFM: Sasa hivi nataka kutoka niende ATM kuchukua pesa, sasa hebu kuwa muwazi tu wangu, kuwa na wewe kwa kama saa tatu utakuwa poa nikupe Sh. ngapi? Mtu mzima nisije nikaumbuka si unajua tena kwa staa kama wewe?

Baby Madaha: Milioni 10!
Frank/OFM: Baby usinikomoe, mimi na wewe tuna safari ndefu, kila nikija Dar tutakuwa pamoja.
Baby Madaha: (...anapiga simu lakini Frank wa OFM hapokei).
Baada ya kuona hivyo, Baby Madaha alituma sms hii “Call” (piga).

MAONGEZI YA SIMU
Frank/OFM: Mambo vipi Baby, habari za muda tena?
Baby Madaha: Salama tu, kwani wewe ulikuwa unataka kutoa sh. ngapi ATM?
Frank/OFM: Mimi ndiyo nilikuwa njiani naelekea ATM natoka hapa hotelini nilipofikia nina Shilingi Mil.4 kwa usiku mmoja, hapo vipi?
Baby Madaha: Katoe 5 fresh, sasa benki gani utaenda kutoa wakati benki zote zimeshafungwa na ATM mwisho kutoa ni Mil.1, sasa hapo itakuwaje?

Frank/OFM: Nitatoa kwa ATM, hata hivyo, nina master-card, naweza kutoa Mil.1 hadi mara 5, usijali kwani pesa kitu gani, cha msingi mimi ni kuwa na wewe!
Baby Madaha: Okay, fine unaweza kuja Kijitonyama (Dar) hapa kwenye hoteli ya (anaitaja jina)?
Frank/OFM: Nimefikia hapa hotelini (jina kapuni), sasa kutoka ni vigumu.
Baby Madaha: Okay, poa nitakuja hapo hotelini saa 1:00 usiku.

Frank/OFM: Usijali karibu sana, nakupenda sana Baby Madaha yaani niko tayari kwa lolote, sema unataka nikupe nini?
Baby Madaha: Hahaha....(anachekaaa) nikija nitakwambia vyote ninavyotaka kwani unafanya biashara gani?

Frank/OFM: Nauza nguo, mara nyingi nafuata Jakarta, Indonesia mara kwa mara lakini natumia muda mwingi kufanya kazi zangu Mwanza.
Baby Madaha: Wee Msukuma eti? Mimi mwenyewe Msukuma kwani unadhani jina Madaha ni la nini hilo, mimi mwenyewe Msukuma.
Frank/OFM: Nimefurahi sana kusikia hivyo, unaweza kuongea Kisukuma?
Baby Madaha: Naweza, wewe nisemeshe tu!
Frank/OFM: Nakutogilwe gete Madaha (Frank anaongea Kisukuma kwamba anampenda sana Madaha)
Baby Madaha: Tukuhoya ntondo nduhu tabu (anajibu kwa Kisukuma kuwa hakuna tatizo tutaongea kesho).

Ulipofika muda waliokubaliana na Frank wa OFM, Madaha alisema kuna foleni kubwa hivyo kuna sababu ya kubadilisha hoteli hiyo iliyoko maeneo ya Ubungo alipopanga Frank wa OFM waonane, Baby Madaha akataka wakutane nyingine iliyoko Kijitonyama.
“Siwezi kuja huko, kwanza kuna mifoleni isitoshe ni vizuri ukafika mwenyewe maeneo haya ya hoteli ya… (anataja), ni sehemu nzuri kwangu hivyo kama huna nia mbaya na mimi ni vizuri ukaja maana kesho nasafiri kwenda Kenya kwenye shughuli zangu za muvi, kwa hiyo unaweza kuja wewe tu maeneo haya,” alisema Madaha.

Frank aliendelea kumbana kwamba tayari alikuwa ameshaandaa pesa shilingi Mil.5, kama walivyokubaliana lakini asingeweza kubeba mfuko wa fedha wote huo isitoshe ni hoteli ambayo ameizoea kwa muda mrefu.
“Ujue Dar mimi siyo mzoefu, achilia mbali kuogopa kutapeliwa hivyo nakuomba uje kwenye hii hoteli nitafurahi sana dear, nakuomba unielewe ujue nakupenda sana mpenzi wangu Baby Madaha, tulia tuyajenge maisha,” alisema Frank wa OFM.

Msanii huyo alimkomalia Frank wa OFM wakutane siku ya Jumanne usiku ambapo alimwambia pia kuwa amepata dharura anakwenda kumuona mfanyabiashara mwenzake kwenye hoteli moja iliyopo Masaki (jina tunalo) ambapo Baby Madaha alitaka waonane na Frank wa OFM kwenye hoteli hiyohiyo.
“Nimepata dharura sitaweza kuonana na wewe, naenda kumuona mfanyabiashara mwenzangu maeneo ya hoteli…(jina tunalo), tuonane kesho muda wa asubuhi,” alisema Frank.

Baadaye Frank alimjulisha mteja wake kuwa yuko njiani anafuata mzigo bandarini akitoka wataonana na Baby Madaha kesho yake asubuhi ya Jumatano iliyopita, alituma sms hii;
Baby Madaha: Kuna stage tano in anything, nakupa tatu, coz uko siku ya tatu, denying, bargaining, accepting..... tomorrow if you be still on game, i give you the remained good day, enjoy Mr Frank, ukitoka cargo call me, we meet!
Frank/OFM: Okay, siku njema nitakutafuta.

Baby Madaha: Matajiri wengine hawana maneno kama wewe kwa mfano…(anataja jina la pedeshee mmoja maarufu Dar). Wanatuma pesa na siyo maneno, wee tuma hela (-)-pesa ipo kila sehemu we tuma ndo nitaweza kujiongeza kama nakuja au laa.
Frank/OFM: Nakutumia muda siyo mrefu, usijali.

IJUMAA LAMBANA BABY MADAHA
Hata hivyo, Baby Madaha hakutumiwa pesa alizotaka ili kukamilisha zoezi badala yake, OFM walitua mzigo wa ushahidi kwenye dawati la Ijumaa ambalo lilikuwa na jukumu la kutafuta mzani wa ishu hiyo.
Ijumaa lilipomtafuta Baby Madaha alikiri kuwa kwenye mawasiliano na mwanaume aliyemtaja kwa jina la Frank Michael Lugisha ambaye alisema alikuwa akifanya naye makubaliano ya kusambaza filamu yake ya The Gal Bladder.

Alipobanwa juu ya makubaliano ya kujiuza kwa mwanaume huyo kwa Sh. milioni 5 alikataa pamoja na kwamba alielezwa kuwa kuna ushahidi wa meseji na sauti.
Alipotakiwa kufika kwenye ofisi za gazeti hili ili kusikilizishwa sauti na kuoneshwa meseji zake, Baby Madaha alisema hawezi kwa kuwa alikuwa na safari ya kwenda nchini Kenya muda mfupi baadaye.

MMMH..PICHAZ...FULL MITEGO NI MTANGAZAJI CLOUDS DIVA LOVENESS LOVE....!

MAZINGIRA YA HIKI CHUO NI BALAA..KAMA SHULE ZA KATA ...WANACHUO WAENDELEZA MGOMO ST. JOSEPH SONGEA


WANACHUO wa Chuo kikuu cha St,Joseph tawi la Songea wamegoma kuingia madarasani na kutoka kufanya shughuli za aina yeyote ndani ya chuo hicho huku wakiwa wamebeba mabango yaliyoandikwa jumbe mbalimbali zikiwemo zilizoandikwa wamechoka kunyanyaswa na wakufunzi ambao wengi wao raia wa India baada ya uongozi wa serikali ya wanachuo kutimuliwa nyazifa zao na kuwasimamisha masomo kwa muda wa miezi sita.

Kundi la waandishi wa habari wa mjini Songea mara tuu baada ya kupata taarifa ya tukio hilo walifika kwenye eneo la chuo kikuu cha St,Joseph kilichopo eneo la Luhuwiko mjini Songea ambako walishuhudia maandamano makubwa ya wanafunzi wakiwa wamebeba mabango yaliyo ujumbe mbalimbali ikiwemo ya wamechoka kunyanyashwa na wakufunzi ambao ni wahindi.

Pia wanachuo hao walishuhudiwa wakiimba nyimbo mbalimbali zenye ujumbe wamechoka kunyanyashwa kwani wao ni watu wazima hapaswi kulinganishwa na wanafunzi wa shule za msingi au sekondari huku wimbo mwingine ukiwa na ujumbe kama siyo mwalimu Nyerere kuleta amani wahindi msingefika kwetu kufanya biashara.

Kufuatia mgomo huo ililazimika askari polisi kufika kwenye eneo hilo huku wakiwa wamebeba silaha kwa lengo la kutuliza gasia ambao walitawanywa katika maeneo mbalimbali ya chuo lakini wanachuo waliendelea na maandamano yao huku wakiimba nyimbo za kushinikiza uongozi wa chuo uwarejeshe viongozi wa serikali ya wanachuo kwa sababu ya kutetea haki za wanachuo ambazo walizodai wahidi hao wamekuwa wakizikiuka. 

Wanachuo hao ambao walidai kuwa malalamiko yao walishayafikisha kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Saidi Mwambungu wakidai kuwa hali ya mazingira ya chuo hicho siyo manzuri lakini bado wahindi hao wameendelea na vitendo viovu licha ya mkuu wa mkoa kuwaangiza kuwa waache kuunyanyasa uongozi wa serikali ya chuo na wayaweke vizuri mazingira ya chuo hicho ikiwa ni pamoja na kufanyia matengezo ya vyoo ambavyo vimesababisha baad hi ya wanachuo kwenda kujisaidia polini.

Walisema kuwa chuo hicho kinavyoo vyenye matundu na wayaweke vizuri mazingira ya chuo hicho ikiwa ni pamoja na kufanyia matengezo ya vyoo ambavyo vimesababisha baadhi ya wanachuo kwenda kujisaidia polini.

Walisema kuwa chuo hicho kinavyoo vyenye matundu 14 ambapo kati ya matundu hayo saba ya wanawake na saba ni wanaume wakati chuo hicho kinawachuo zaidi ya 1,200 na kufanya kusababisha tundu moja kutumiwa na wanachuo 64 badala ya kati 20 au 25.

Kwa upande wa viongozi wa serikali ya wanachuo waliyotimuliwa Aristides Munjwahuzi na waziri mkuu wake Deogratius Sanga waliwaambia waandishi wa habari kuwa matatizo makubwa yaliyopo ndani ya chuo hicho ni mengi ambayo wanachuo wakijaribu kulalamika kupitia uongozi wa serikali ya wanachuo badala yake uongozi wa chuo umefikia kuufukuza uongozi wa serikali ya chuo na kuwasimamisha masomo kwa muda wa miezi sita jambo lilionekana kuwa ni uonevu mtupu. 
Hata hivyo mmoja wa viongozi wa chuo hicho mtawa Antonia Emmanuel alisema kuwa suala la viongozi wa serikali ya wanafunzi la kuvuliwa madaraka na kusimamishwa masomo walishapewa maelekezo kuwa malalamiko yao walete kwa maandishi ili yajadiliwe lakini hawakufanya hivyo jambo ambalo aliliita kuwa ni dharau na badala yake ameshangazwa kuona wanachuo wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali lakini amesema tatizo hilo linahitaji kuwepo mazungumzo ya pande zote mbili yakiwa na lengo la kumaliza tatizo hilo.



Thursday, January 16, 2014

HIVI NDIVYO H.BABA ALIVYOSHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA...TAZAMA MAPICHA HAPA!!!

 

H.Baba na mke wake, Florah Mvungi wakilishana keki.

 
Florah Mvungi akiwa na mtoto wake Tanzanite.H.Baba akimlisha keki mama yake.
 IMG-20140115-WA0068

Mke wake H.Baba, Florah Mvungi  akiwa ameshika keki ya bethidei.
IMG-20140115-WA0069
H.Baba akiwa na mtoto wake.
IMG-20140115-WA0070
Florah Mvungi akimlisha keki mtoto wake Tanzanite.
IMG-20140115-WA0071 IMG-20140115-WA0072

Jana tarehe mtu mzima H.Baba msanii kutoka kule Mwanza alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa na familia yake nikimaanisha mke wake na mtoto wao mpya anaitwa Tanzanite pamoja na mama mzazi wa HBaba na wadogo zake wa mwisho.

 Hizi ni baadhi ya picha tu wakiwa pamoja wakila keki kwa pamoja.

JACKIE CLIFF ARUDI URAIANI??? HIKI NDIO ALICHOPOST INSTAGRAM MUDA MCHACHE ULIOPITA!

Sijui ni ka mchezo gani ila ndio hivyo Jack Cliff anaye semekana alikamatwa na madawa ya kulevya chini amepost picha hiyo kwenye instragram yake.....Hata masogange ilikuwa hivi hivi alianza kupost post picha zake mara tukasikia kaachiwa.

HIVI NI JINSI FERUZI ALIVYODAKWA NA BANGI NA KUTIWA MBARONI

NYOTA aliyetamba katika muziki wa kizazi kipya enzi hizo akiwa na Kundi la Daz Nundaz, Ferooz Mrisho, juzikati alikamatwa na polisi na kutupwa lupango katika Kituo Kidogo cha Mabatini, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, baada ya kukutwa akivuta bangi pamoja na vijana wenzake kadhaa maeneo ya Sinza, karibu na Baa ya Meeda.
Mwanamuziki Ferooz Mrisho akiwa mikononi mwa polisi baada ya kunaswa akivuta bangi.
Habari zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda na baadaye kuthibitishwa na gazeti hili, zilisema Ferooz alikuwa akivuta bangi katika eneo hilo kabla ya majirani wanaokerwa na tabia hiyo, kupiga simu polisi wakitaka kukomeshwa kwa jambo hilo.
“Hapana tumechoka na tabia zao, kila ukipita hapa unakula ‘marashi’ ya bangi tu, vilevile sisi tuna vijana wa rika lao, hawa vijana wanaopita hapa wanasoma,  tunaogopa sana wasije wakajiunga na wao hapa kula ganja,” alisema mama mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
Ferooz akiwa amepigwa pingu na mwenzake.
Ilidaiwa kuwa msanii huyo pamoja na wenzake wamekuwa na kawaida ya kukaa katika kijiwe hicho kila siku na kuvuta bangi huku baadhi yao wakitumia madawa ya kulevya.
Baada ya kutiwa nguvuni kwa vijana hao, wakazi wa maeneo hayo wamewamwagia sifa Mkuu wa Kituo cha Polisi Mabatini aliyefahamika kwa jina moja la Mapunda kwa jinsi alivyofanikisha askari kuwahi eneo hilo la tukio.
...Akishushwa kutoka kwenye gari.
“Tulipopiga simu polisi, hatukutegemea kama ingekuwa haraka hivyo, tunashangaa baada ya muda mfupi, wakaja eneo hili, kwa kweli huyu mkuu ni mfano wa kuigwa, maana siku hizi likitokea tukio lolote lile ni dakika chache gari limefika,” alisema mkazi mmoja wa eneo hilo.
Ferooz, mkali wa kibao cha Starehe baada ya kufikishwa kituoni hapo alichukuliwa maelezo yake kabla ya kuwekwa rumande. Hadi gazeti hili likienda mitamboni haikufahamika siku ya kufikishwa mahakamani kwa wahalifu hao.

WEMA ANYANG'ANYWA KILA KITU, KISA KURUDIANA NA DIAMOND,KIGOGO ACHUKUA HADI NYAYA KWENYE OFISINI KWAKE

ZILE tambo, mbwembwe na majigambo ya Miss Tanzania 2006/07, aliye pia msanii wa filamu Bongo, Wema Isaac  Sepetu, zimefika mwisho kufuatia kunyang’anywa samani za ofisi yake ya Endless Fame Film Production na aliyekuwa mpenzi wake, Clement ‘kigogo wa ikulu’ na sasa amebaki mweupe,  Amani limepakuliwa ikiwa imeiva.
Wema Isaac  Sepetu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo la aibu lilijiri hivi karibuni kwenye ofisi hiyo ya Wema iliyopo Mwananyamala-Komakoma jijini Dar.
KIGOGO WA IKULU AVAMIA NA MABAUNSA
Habari za uhakika zinadai kuwa, siku ya tukio, Clement akiwa ameongozana na watu waliosadikiwa kuwa ni mabaunsa, walivamia ofisi hiyo aliyomfungulia mlimbwende huyo na kukomba vitu vyote vya thamani alivyomnunulia wakati wa mapenzi motomoto (hakuna lenye mwanzo lisilo na ncha).
KUMBE ALIKODI CANTER
Kama njiwa apelekaye ujumbe muhimu wa huba, mtoa taarifa huyo alizidi kumwaga ‘upupu’ kuwa, siku hiyo Clement mbali na gari lake la kifahari, pia alitinga akiwa na gari aina ya Canter ambapo bila maswali wala maelezo achilia mbali ufafanuzi, alikusanya vifaa vyote na kuvirundika kwenye gari.
Wema akiwa katika ofisi yake kabla ya kunyang'anywa samani zilizomo.
IDADI YA VITU VILIVYOBEBWA
Vifaa hivyo ni tarakishi (computer), kamera ya kurekodi sinema (video camera), vifaa vya kurekebisha hali ya hewa (air conditioner), vifaa vya kuhifadhia umeme wa ziada, uninterruptible power supply  (ups) pamoja na vifaa vingine zikiwemo nyaya za umeme na kuiacha ofisi nyeupe kama uwanja wa mpira.
“Hali ni mbaya sana, jamaa (Clement) alichukua kila kitu ndani ya ofisi hiyo kuanzia kompyuta, kamera hata nyaya! Hivi tunavyoongea, ofisi haina kitu kabisa,” kilisema ‘kikulacho’ hicho.
CHANZO NI DIAMOND
Mpashaji huyo alizidi kuyapa utulivu masikio ya mwandishi wetu kuwa, chanzo cha kigogo huyo kufanya ‘umafia’ huo ni kitendo cha Wema kurejesha penzi lake kwa ‘mtemea maiki’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’.
Ofisi ya Wema kwa ndani.
Taarifa hizo zilieleza kuwa, kitendo hicho kilichochea hasira za Clement, hasa pale Diamond alipohojiwa kuhusu kuingilia penzi hilo na kujibu hamwogopi mtu, “ndiyo maana Clement akaamua kumwaga ugali baada ya wawili hao (Wema na Diamond) kumwaga mboga,” kiliongeza chanzo.
HEBU MSIKILIZE WEMA
Ili kujua yapi ni maziwa na lipi ni tui juu ‘niuz’ hizo, mwandishi wetu alimtafuta Wema na kukutana naye laivu juzi ambapo alikiri kukumbwa na zahama hiyo huku akionesha mshangao wa wazi kwa kitendo alichofanyiwa na ‘zilipendwa’ wake huyo.
Geti la kuingia katika ofisi hiyo.
“Ni kweli kabisa Clement amefanya hivyo, lakini nashangaa na ni mara yangu ya kwanza kuona wapenzi wakiachana mwanaume anaamua kuchukua vitu vyote alivyowahi kumnunulia au kumpa.
“Huo ni ushamba na unyanyasaji, akumbuke kwamba alipokuwa na mimi alinitumia pia,” alisema Wema na kuongeza:
“Hata hivyo, namshukuru Mungu, vitu vyote alivyochukuwa Clement, baby (Diamond) kasema ataninunulia, wiki mbili hazitapita.”
Wema alikwenda mblele zaidi kwa kuonesha machungu yake kwa kigogo huyo pale aliposema: “Kwanza nasikia vitu vyenyewe alipofika nyumbani kavimwaga nje maana ndani hakuna nafasi.”
Wema akiwa na mpenzi wake Diamond aliyesababisha mpaka akanyang'anywa samani hizo.
KAANZA MWAKA VIBAYA
Mwanzoni mwa mwaka huu, Wema alikumbwa na mkasa wa kunyang’anywa lile gari la kifahari alilodai ni lake, Audi Q7 baada ya kusemekana kuwa halikuwa lake.
Kumbe gari hilo alipewa na Clement ambaye naye alilikopa kwa thamani ya shilingi milioni 90 kutoka kwa mtu aliyejulikana kwa jina la Shadrack Tweve.
Tweve, baada ya kuzungushwa sana kulipwa fedha hizo, alikimbilia Mahakama ya Wilaya ya Ilala ambapo hakimu aliamuru gari hilo likamatwe na kurejeshewa mlalalamikaji huyo.
PENZI LA WEMA, KIGOGO WA IKULU
Uhakika ni kwamba, penzi kati ya Wema na kigogo huyo halipo tena na kwa sasa jamaa ana demu mwingine (jina tunalo) ambapo mapaparazi wetu wanaendelea kufuatilia kwa karibu ili kuwanasa katika mazingira yoyote yale.

.FLORA MVUNGI ATOA YAKE YA MOYONI KUHUSU PENZI LA WEMA SEPETU NA DIAMOND........




LAANA....!! MTOTO WA KIGOGO ATUPIA PICHA ZA UTUPU MTANDAONI...ZITAZAME HAPA, NI AIBU TUPU..

Wakati sakata la mastaa kupiga picha za chafu likiwa bado halijaondoka vichwani mwa watu, gazeti la Ijumaa limenasa picha nyingine zinazomwonesha binti aliyetajwa kwa jina moja la Tuma akiwa mtupu ambaye inasemekana ni mtoto wa kigogo mmoja mkoani Morogoro, shuka mstari kwa mstari.

Awali gazeti lenye heshima tele mbele ya jamii, Ijumaa lilipokea waraka pepe kutoka kwa msomaji mmoja mkoani Morogoro ambaye alisema, anazo picha chafu za binti huyo zinazosambazwa kwa kasi ya moto wa petroli kwenye mtandao wa intaneti. Waraka pepe uliotumwa kwenye anuani pepe ya Ijumaa ilisomeka: “Hello Ijumaa, ninazo picha za Tuma. Yupo mtupu, amelala kitandani, kama mnahitaji hiyo habari, nipeni pesa niwape mchongo mzima.” 
 Kwa kutambua umuhimu wa habari hiyo, haraka, gazeti hili lilijibu waraka pepe wa ‘sosi’ huyo na baada ya makubaliano, alituma picha za mapozi tofauti za mrembo huyo (kama zinavyoonekana ukurasa wa mbele) na maelezo kwa ufupi. Chanzo hicho, kilieleza kwamba, picha hizo zinadaiwa kupigwa katika hoteli moja yenye jina kubwa jijini Tanga, ingawa haikujulikana ni nani aliyempiga na alikuwa na nia gani. 
Alidai kwamba, kwa sasa picha hizo siyo stori tena Morogoro, kwasababu zimezagaa kila kona ya ‘Mji Kasoro Bahari’. 
“Huku hakufai, mchezo aliofanyiwa ni mchafu na Tuma anahaha kila kona, amefedheheka sana, anaogopa kuchafua familia yake,” kiliendelea kupasha chanzo hicho.

Katika picha hizo, zipo zinazomwonesha binti huyo mrembo akiwa amepozi mwenyewe kitandani na kanga moja, wakati nyingine zikimwonyesha amelala mtupu, uso wake ukipambwa na tabasamu mwanana, tukio linaloashiria kwamba alikuwa akitoa ushirikiano wa kutosha wakati zoezi la kupigwa picha hizo lilipofanyika. 
Aidha, ipo picha inayomwonesha binti huyo akiwa analia, huku sababu za kilio chake akiwa anazijua mwenyewe.
Hakuna maelezo ya kutosha juu ya picha hizo ila Timu ya Ijumaa inaingia mzigoni ili kubaini upande wa pili kisha tutawaletea mwendelezo wake.
KUTOKA KWA MHARIRI
Kwa muda mrefu sasa, magazeti pendwa yamekuwa yakiripoti habari zinazohusu wasichana kupiga picha za utupu kwa lengo la kukemea tabia hiyo, lakini bado sikio la kufa halisikii dawa kwani ndiyo kwanza wamecharuka. 

Kwetu sisi, kupiga picha chafu si tabia njema na inaharibu maadili ya jamii nzima ambayo kimsingi si utamaduni wetu.
Tunarudia tena na tena kutoa angalizo letu kwa mabinti kuwa makini na wapenzi wao, wasikubali kupigwa picha chafu wanapokuwa nao faragha, kwani inaweza kuharibu

Saturday, January 11, 2014

WAKATI JACK AKIWA BADO KAKAMATWA NA MADAWA CHINA....AGNESS MASOGANGE ANASWA NA JUX KATIKA POZI LA KIMAHABA...

VIDEO Queen, Agnes Jerald ‘Masogange’ hivi karibuni alibambwa maeneo ya Sinza Kamanyola jijini Dar akijiachia na anayetajwa kuwa ni mpenzi wa Jack Patrick, Juma Khalid ‘Jux’.
Masogange akipozi na Jux.
Wawili hao walibambwa kwenye duka moja lililopo maeneo hayo baada ya Jux kutua kutoka China huku Agnes akionekana kama anayemfariji kwa tukio la Jack kunaswa na madawa ya kulevya.
http://api.ning.com/files/Iht4Psekqy0wttdXe*EsPRkqo*eRW*Qp69gUzbFS7smv8PTpbqof801LuB2JiAsnEHN0DmKCmtkMNQ9uNA-PB4Cq4PCBRIbh/jacknajux.jpg%3Fwidth%3D650Jux akiwa na mpenzi wake Jack Patrick.
Akiuzungumzia ukaribu wake na Jux, Masogange alisema: “Wala hakuna lolote kati yangu na yeye. Mimi na wale akina Jux pamoja na dada yake ni watu wangu wa karibu sana tunaojuana muda mrefu hivyo tulikuwa  tunabadilishana mawazo tu.”
Masogange akiwa na Jack.
Jux na Jack wamekuwa wakionekana katika mitaa ya China wakila bata huku kukiwa na madai kuwa ni wapenzi na kuonekana kwa Jux na Masogange wakijiachia kumeibua maswali mengi.

-GPL