Mastaa
wa filamu za Kibongo wenye jina kubwa mjini, Aunt Ezekiel, Jacgueline
Wolper na Snura Mushi hivi karibuni walitisha kwa kufunga mtaa kutokana
na mauno waliyokuwa wakikata mbele za wapiga ngoma wa Kundi la Baikoko,
tukio lililojiri Mwananyamala, Dar nyumbani kwa msanii mwenzao Vanitha
Omary.
“Yaani wewe ulikosa mambo, Snura alitoa shoo na mapacha wake utadhani alikuwa amelipwa, yaani walinogesha ngoma ya kumuaga mdogo wake Vanitha ambaye anakwenda kufunga ndoa Dodoma,” alisema sosi aliyekuwa akimsimulia mwandishi wetu.
Aidha, wageni waliokuwa wamealikwa eneo hilo hawakudhani kama Wolper na Aunt wangeweza kujituma vile kama walivyokuwa wakikata mauno hayo kwa sababu ustaa wote waliuweka pembeni na kujiachia kwa raha zao.