
‘Yeah ilikua mwaka 2003 baada ya Jay Moe kumwambia unafanana sana na dogo alisema ndio kweli nafanana nae lakini mtu aliekuja kunifahamisha zaidi ni Dully,Dully alisema unafanana sana na Ngwea na mpaka leo huwa ananiita Ngwea.watu walinishawishi kulingana na hii sura nliyonayo watu wamenishawishi taratibu naanza kuingia kwenye game bado sijafanya track nipo njiani,nakutana na vituko vingi wengine wananikimbia wanasema nimefufuka na vitu vingine vya ajabu nakutana navyo mtaani muda mwingine nasisimka nahisi kama Mangwea yuko ndani ya mwili wangu,naweza kuimba baadhi ya ngoma za Ngwea kama tupo juu..na baadhi ya ngoma zingne.
Nikaona si mbaya tukafahamu hata kwa uchache historia yake na anamjua vipi Marehemu Ngwea.


