Eliasi Mokiwa mwandishi anaedaiw kupigwa akiwa kazini na walinzi wa Gwajima
Mchungaji
Josephat Gwajima na wasaaidizi wake wameingia kwenye kashfa nzito ya
kumshambulia mwandishi wa habari Mkoani Tanga Ndugu Eliasi Mokiwa hadi
kumtengua kiuno chake kisa kikiwa kuwapiga picha misukule wake aliodai
kuwagomboa mikononi mwa wachawi wa Tanga.
Habari
za uhakika zilizothibitishwa na mwandishi wetu aliyekuwepo eneo ya
tukio huko Mkoani Tanga ambako Gwajima na wafuasi wake waolikuwa
wakifanya hudia misukule.
Akizungumzia
tuki hilo mwandish huyo ambae anaripotia gazeti la Jibu la Maisha
lakini ni mwanafunzi wa chuo cha Royal College ngazi ya Cheti kilichopo
Mkoani humo alisema ilikuwa siku ya tarehe moja desemba 2013 saa kumi za
jioni aliwa na mwandishi wa gazeti hili Mkoani Tanga Bwa Sadiki Amidu
na wakiwa kwenye viwanja vya Tangamana wakati mchungaji huyo akitangaza
kuwa kuna msukule amedondoka katikati ya watu.
Mwandishi
huyo anasema alisogea na yeye ili kushuhudia msukule huyo pamoja na
kumpiga picha lakini katika hali isiyotarajia baada ya kupiga picha moja
alishtuka amepaishwa juu kumbe kuna msaidizi wa Gwajima ambae alimpiga
mtama ulimpaisha kimo cha ng’ombe na kudondoke kiuno.
Mara
baada ya kutua nchini mwandishi huyo anasema alisikia kitu flani
kimelia kwenye kiuno chake kumbe nyonga ilikuwa imeshateguka ambapo
wakati akigragara chini walikuwa wasaidiz wanne na walimbeba juu hadi
nyuma ya jukwaa na kuanza kumsurubu, wakati huo Mchungaji Gwajima
alikuwa anashuhudia mchezo mzima bila kutoa kauri yeyote.
Mwandishi
huyo aliendelea kueleza “ Nilipigwa sana huku wakinisachi mifukoni na
kunichukulia pesa yangu yote ambayo ilikuwa ni shilingi elfu tano ya
nauli huku wengine wakiniuliza kama pesa nyingine nimeweka wapi lakini
kiwajibu kuwa sina pesa nyingine na kuwaeleza mimi ni mwandishi wa
habari hivyo wasinidhalilishe kiasi hicho lakini hawakutaka kusikia”
Alisema Eliasi
Hata
hivyo Eliasi aliendelea kusema kuwa “ Mwandishi mwezangu baada ya kuona
vile alitimua mbio kuokoa maisha yake kwani walishashtukia kuwa tuko
wawili hivyo huenda wangetukamata wote, baadae alikuwa mchungaji mmoja
mwanamke ambae sikufahamu labda huenda alikuwa mke wa Gwajima kutokana
na heshima waliyompa muda ule kwani wakiwa bado wananishambulia kwa
ngumi za chembe na walipomuona mama huyo waliniacha haraka na kuganda”
Alisema mwandishi huyo
Baada
ya mama huyo kuuliza kosa langu nini wakamueleza kuwa kuwa mimi
nimepiga picha misukule na nilikuwa navizia watu waliokaa uchi na
kuwapiga pamoja na misukule yao, ambapo mama huyo aliamuru niachiwe huru
lakini kama hizo picha za misukule zipo kwenye kamera yangu zifutwe
halafu wanirusu na mama huyo aliangalia kwenye kamera na kukuta hamna
picha yoyote ya aina hiyo.
Hata
hivyo Eliasi aliendelea kusema “Nilivyoachiwa huku nikiwa
nyang’anyang’a nilijisogeza kidogo kidoga hadi kituo kikuu cha Polisi na
kutoa taarifa na wakampatia Jarada la Upelelezi PE namba 71 -2013
pamoja PF3 ambapo alikwenda kwenye Hospitali ya Jiji ambako walimpatia
matibabu hadi siku iliyofuta ambapo alirudi na ile PF3 tena Polisi.
Aidha
kutokana na mkutano huo kuwa isku ya mwisho kwenye viwanja hivyo na
wakahitaji kuongeza siku za mkutano lakini walizuiwa kibari badara yake
walihamishia mkutano huo kwenye viwanja vya Ridochi. Na baada ya siku
mbili Polisi wakiwa na Deffender walikwenda kuvamia mkutano huo kwa
lengo la kuwakamata wale wote walihusika na tukio la kumpiga na kujeruhi
mwandishi huyo, lakini kwa bahati mbaya mwandishi huyo akiwa
ameandamana na Askari hakuwata wale walimpiga hivyo na kufanya Polisi
kuendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Baada
ya taarifa hizo Maskani Bongo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga “RPC”
Masawe ili kuzungumzia ishu hiyo ambapo alipatikana lakini kwa bahati
mbaya akajibu kuwa yuko kwenye mafunzo Moshi hiyo tumtafute Kaimu wake
ambae nae alipopigiwa simu simu hiyo iliita tu bila kupokelewa.
Misukule
ya mchungaji Gwajima imekuwa na utata mkubwa sana kwenye jamii kutokana
na wengi kuamini kuwa ni propaganda tu za kujizolea waumini, kwa mfano
misukule wote aliowatoa Mkoani Tanga wanadaiwa ni wa kutengenezwa ndiyo
maana amekuwa mkali kwa waandishi ili wasije kuripoti uwongo huo.
Hata hivyo kwa wakazi mji wa Tanga wamesikitishwa na tukio hilo na kupigwa kwa mwandishi huyo maarufu ambae ni ndugu moja na mtangazaji wa TBC1 Domonic Mokiwa
