Wakati
ambapo zimebaki siku chache tu hadi tusherehekee sikukuu ya Christmas,
mastaa wengi duniani wamekuwa wakishare kadi zao spesho za Christmas
zenye picha zao pia. Kwa Nigeria tayari Iyanya amefanya hivyo.

Lakini damu ya kunguni ya Diamond Platnumz yenye harufu kali ipitapo jirani na pua za ‘haters’ wengi wa Kibongo, imemponza baada ya kuweka picha ya kadi ya Christmas kwenye ukurasa wake wa Facebook. Haijulikani lakini kama ni kadi ama ni teaser ya kampeni yake kama balozi wa Cocacola. Haikuchukua muda, baadhi ya mashabiki wake wakaanza kuicheza kadi ya ‘udini’.
ZIfuatazo ni baadhi ya Comments za mashabiki hao...