Kijana Abel Dafe 21, (pichani) mkazi wa
Kayenze, Mwaloni jijini Mwanza amezua sintofahamu ya aina yake baada ya
kudaiwa kufariki dunia na maiti yake kuzikwa wiki chache zilizopita na
baadaye kuonekana akiwa hai, bali denti wa Chuo cha Biashara (CBE) Tawi
la Mwanza ndiye akidaiwa kufa.
Desemba 2, mwaka huu, Abel alidaiwa
kufa maji akiogelea katika Ziwa Victoria na mwili wake kuthibitishwa na
mjomba’ake, mwili ukapelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kabla ya
kusafirishwa Sengerema kwa maziko Desemba 4.
Akizungumza na waandishi wetu juzi, mtu
wa karibu wa Abel aliyejitambulisha kwa jina la Emmanuel alisema baada
ya kumaliza mazishi, familia ilirudi Kayenze, Lakini yeye Desemba 17
mwaka huu ghafla alionana na Abel akiwa mzima wa afya maeneo ya Mwaloni.
Alisema alimuweka chini ya ulinzi na
kumpeleka Kituo cha Polisi cha Kayenze na kutoa taarifa kwa ndugu
waliokuwa Sengerema ambao walifika na kujionea marehemu akiwa hai!
Kituoni hapo, Abel alikataa katakata kuwa yeye hakufa alikuwa kwenye misele yake ila alipoteza simu ndiyo maana hakuwa na mawasiliano na nduguze.
Kituoni hapo, Abel alikataa katakata kuwa yeye hakufa alikuwa kwenye misele yake ila alipoteza simu ndiyo maana hakuwa na mawasiliano na nduguze.
Ndugu hawakuyaamini mwaelezo hayo,
wakati mwingine walitaka asiwakaribie maana ni mzimu, lakini wakiwa
katika maswali mengi juu ya Abel yupi aliyezikwa, walipata taarifa
kituoni hapo kuwa maiti waliyemzika Sengerema anaitwa Manyama Chimwejo
na nduguze wamepatikana.
Polisi wakaitaka familia hiyo ya Abel
kukaa na familia ya Manyama kujadili hatima, kama watafukua maiti hiyo
na kwenda kumzika upya Kigoma au watamwacha hukohuko Sengerema
alipozikwa awali.
Akizungumza kwa simanzi, Abel (aliyedhaniwa kufa) alisema ndugu zake wanachojua waliyemzika ndiye Abel bali amefufuka.
“Ndugu zangu hawaamini kama mimi ni mzima hivyo napata tabu sana kwa kuwa kila mtu ananipigia simu kuniuliza. Mimi sikufa, nilikuwa nyumbani kwangu, tatizo lilikuwa ni mawasiliano, nilipoteza simu,” alisema Abel.

Kwa upande wa pili, kaka wa marehemu
aliyejitokeza kudai maiti ya mdogo wake aliyezikwa kimakosa
aliyejitambulisha kwa jina la Christopher Chimwejo alimtaja Manyama
Chimwejo (20) kuwa kweli alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE),
Tawi la Mwanza mwaka wa kwanza na alifika kuishi naye mapema mwezi huu
baada ya chuo kufungwa.
Alisema Manyama alitoweka nyumbani
kwake ghafla maeneo ya Mwaloni na baada ya hapo hakumuona tena jambo
lililomfanya atoe taarifa polisi.
Hata hivyo, sakata hilo lilimalizika Desemba 21, mwaka huu katika Kituo cha Polisi Kirumba D ambapo pande zote mbili zilikutana na kukubaliana kuacha kaburi la marehemu Manyama liendelee kuwa Sengerema licha ya kwamba familia hiyo haiamini kama mwanafunzi huyo alifariki dunia.
“Hapa
kuna kitu, sisi hatujafiwa na ndugu yetu, tumechezewa. Kama ndugu yenu
aliyekufa amerudi hata ndugu yetu pia atarudi tu, ngojeni kwanza
tukatambike kwetu Kigoma,” alisema kaka huyo wa marehemu.