WANANCHI
wenye hasira kali wamempiga hadi kumuua mtu mmoja mwanaume
aliyesadikiwa kuwa ni mchawi baada ya kuanguka akiwa amepanda ungo
maeneo ya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, Mtanzania limeshuhudia.
Kijana
huyo mkazi wa Mwanza anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi
25, alianguka jana saa 12 asubuhi maeneo hayo baada ya kudai kuwa
alikuwa kwenye safari zake za kishirikina.
Kabla ya kufariki alisema
“mimi nilikuwa na wenzangu sita, wanaume watatu na wanawake watatu
ambapo tulikuwa tunatoka Mwanza kuelekea kwenye mkutano wetu”.
“Lakini
mimi kwa bahati mbaya nilikiuka masharti tuliyopewa na mkuu kwa
kufungua macho ndipo ghafla nilianguka na kupata kadhia hii inayopelekea
mauti yangu”.
Hata
hivyo kutokana na vurugu zilizokuwapo eneo hilo la tukio, ambapo
wananchi wa eneo hilo walikuwa wanataka kumuua, kijana huyo alishindwa
hata kutaja jina lake kutokana na kipigo alichokuwa anakipata kutoka
kwao.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wengine wa tukio hilo walisema baada ya kuanguka
eneohilo walimkimbiza hadi ndani kwa mtu na kumtoa pamoja na zana zake
za kichawi ambapo walizichoma kwanza moto ikiwa pamoja na ungo wenyewe
ndipo wakaendelea kumpiga kwa mawe hadi mauti yalipomkuta.
“Huyu
jamaa bwana, ameanguka hapa, sasa kwakuwa sisi hatuna mzaha na watu
kamahawa tumemtoa huko alikokimbilia na kumhalalisha kwa vijana wa kazi
hapa baada ya kuhakikisha zana zake zote tumezichoma moto” alisema mkazi
mmoja wa maeneo hayo.
Hata
hivyo baadhi ya wananchi walielekeza lawama zao kwa Jeshi la Polisi
(Kituo cha Polisi Kimara) kilichopo Mbezi kwa Yusuph kwa kuchelewa kuja
kumuokoa kija huyo ingawa walipewa taarifa mapema.
“Sisi
tumepiga simu kituoni hapo hata kabla huyu mchawi hajaanza
kushambuliwa, lakini angalia tukio limeanza saa 12 asubuhi wanakuja
baada ya masaa mawili, huu nu uzembe” alisema mkazi wa eneo
hiloaliyejitambulisha kwa jina moja la Ali
Ingawa katika tukioa hilo
kulitokea mkazi mmoja aliyekuwa na silaha aina ya bastola na kufyatua
risasi hewani kwa lengo la kuwatawanyisha wananchi hao wenye hasira
kali, haikusaidia kitu kwani waliendelea kumpiga hadi wakahakikisha
amekufa.
Mtanzania
lilibisha hodi katika kituo cha Polisi Kimara ambacho mwili wake
ulipelekwa ili kupata uthibitisho zaidi lakini askari wa zamu waliokuwa
mapokezi walisema hawana mamlaka ya kutoa maelezo hadi mkuu wa kituoa au
mkuu wa makosa ya kieupelezi wa kituo hicho ndiyo wenye dhamana.
Aidha
wakuu hao OC CID (ASP) M. Mganga pamoja na Mkuu wa kituo wote
hawakuwapo kituoni wakati Kamanda wa kipolisi wa Kinondoni, Elias
Kalinga hakuweza kupatikana ili kudhibitisha tukio hilokutokana na namba
yake ya simu kuita bila kupokelewa.
Wakazi wa Mbezi Luis, wakimshambulia mchawi huyo.
Kipigo kinaendelea hadi kupelekea umauti wake.
Wakimsindikiza kuelekea katika mtaro ambao walimpiga na bonge la kitofa na kumuua.