WANACHUO wa
Chuo kikuu cha St,Joseph tawi la Songea wamegoma kuingia madarasani na
kutoka kufanya shughuli za aina yeyote ndani ya chuo hicho huku wakiwa
wamebeba mabango yaliyoandikwa jumbe mbalimbali zikiwemo zilizoandikwa
wamechoka kunyanyaswa na wakufunzi ambao wengi wao raia wa India baada ya uongozi wa serikali ya wanachuo kutimuliwa nyazifa zao na kuwasimamisha masomo kwa muda wa miezi sita.
Kundi
la waandishi wa habari wa mjini Songea mara tuu baada ya kupata taarifa
ya tukio hilo walifika kwenye eneo la chuo kikuu cha St,Joseph
kilichopo eneo la Luhuwiko mjini Songea ambako walishuhudia maandamano
makubwa ya wanafunzi wakiwa wamebeba mabango yaliyo ujumbe mbalimbali
ikiwemo ya wamechoka kunyanyashwa na wakufunzi ambao ni wahindi.
Pia
wanachuo hao walishuhudiwa wakiimba nyimbo mbalimbali zenye ujumbe
wamechoka kunyanyashwa kwani wao ni watu wazima hapaswi kulinganishwa na
wanafunzi wa shule za msingi au sekondari huku wimbo mwingine ukiwa na
ujumbe kama siyo mwalimu Nyerere kuleta amani wahindi msingefika kwetu
kufanya biashara.
Kufuatia mgomo huo ililazimika askari polisi
kufika kwenye eneo hilo huku wakiwa wamebeba silaha kwa lengo la
kutuliza gasia ambao walitawanywa katika maeneo mbalimbali ya chuo
lakini wanachuo waliendelea na maandamano yao huku wakiimba nyimbo za
kushinikiza uongozi wa chuo uwarejeshe viongozi wa serikali ya wanachuo
kwa sababu ya kutetea haki za wanachuo ambazo walizodai wahidi hao
wamekuwa wakizikiuka. Wanachuo
hao ambao walidai kuwa malalamiko yao walishayafikisha kwa mkuu wa mkoa
wa Ruvuma Saidi Mwambungu wakidai kuwa hali ya mazingira ya chuo hicho
siyo manzuri lakini bado wahindi hao wameendelea na vitendo viovu licha
ya mkuu wa mkoa kuwaangiza kuwa waache kuunyanyasa uongozi wa serikali
ya chuo na wayaweke vizuri mazingira ya chuo hicho ikiwa ni pamoja na
kufanyia matengezo ya vyoo ambavyo vimesababisha baad hi ya wanachuo
kwenda kujisaidia polini.
Walisema kuwa chuo hicho kinavyoo
vyenye matundu na wayaweke vizuri mazingira ya chuo hicho ikiwa ni
pamoja na kufanyia matengezo ya vyoo ambavyo vimesababisha baadhi ya
wanachuo kwenda kujisaidia polini.
Walisema kuwa chuo hicho
kinavyoo vyenye matundu 14 ambapo kati ya matundu hayo saba ya wanawake
na saba ni wanaume wakati chuo hicho kinawachuo zaidi ya 1,200 na
kufanya kusababisha tundu moja kutumiwa na wanachuo 64 badala ya kati 20
au 25.
Kwa upande wa viongozi wa serikali ya wanachuo
waliyotimuliwa Aristides Munjwahuzi na waziri mkuu wake Deogratius Sanga
waliwaambia waandishi wa habari kuwa matatizo makubwa yaliyopo ndani ya
chuo hicho ni mengi ambayo wanachuo wakijaribu kulalamika kupitia
uongozi wa serikali ya wanachuo badala yake uongozi wa chuo umefikia
kuufukuza uongozi wa serikali ya chuo na kuwasimamisha masomo kwa muda
wa miezi sita jambo lilionekana kuwa ni uonevu mtupu. Hata
hivyo mmoja wa viongozi wa chuo hicho mtawa Antonia Emmanuel alisema
kuwa suala la viongozi wa serikali ya wanafunzi la kuvuliwa madaraka na
kusimamishwa masomo walishapewa maelekezo kuwa malalamiko yao walete kwa
maandishi ili yajadiliwe lakini hawakufanya hivyo jambo ambalo aliliita
kuwa ni dharau na badala yake ameshangazwa kuona wanachuo wakiwa
wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali lakini amesema tatizo hilo
linahitaji kuwepo mazungumzo ya pande zote mbili yakiwa na lengo la
kumaliza tatizo hilo.
Saturday, January 18, 2014
MAZINGIRA YA HIKI CHUO NI BALAA..KAMA SHULE ZA KATA ...WANACHUO WAENDELEZA MGOMO ST. JOSEPH SONGEA
Unknown
BONGO