Mwishoni mwa wiki iliyopita, taarifa zilienea katika mitandao ya
kijamii na vyombo mbalimbali vya habari Bongo kwamba msanii wa Bongo
Fleva, David Genzi ‘Young Dee’ na nyota wa filamu, Elizabeth Michael
‘Lulu’ wamebambwa na polisi wa doria wakivunja amri ya sita ndani ya
gari aina ya
Hyundai, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, tukio lililojaa
utata mkubwa.

Kwa mujibu wa habari hizo, wawili hao walinaswa wakifanya uchafu huo
na askari waliokuwa doria lakini wakawavuta pembeni na baada ya muda,
wakawaachia na kutokomea kusikojulikana.
Ili kupata ukweli wa tukio hilo la aibu, mwandishi wetu alianza kwa
kumvutia waya Young Dee na kumsomea mashtaka yake ambapo alifunguka kuwa
ni kweli amezisikia habari hizo lakini akakana kwamba ishu hiyo siyo ya
kweli bali imezushwa na kundi la watu wenye lengo la kumharibia jina
lake mbele ya jamii.
“Siyo kweli kabisa, isitoshe nina kama mwezi mzima sijaonana na huyo
Lulu, huku ni kutaka kuchafuliana majina tu,” alisema Young D.
Habari zinadai kuwa licha ya Young Dee kukanusha kuwa hajaonana na
Lulu kwa muda mrefu, siku ya tukio walikuwa pamoja ingawa hawakutaka
kuonekana na mtu yeyote.
Kwa upande wa Lulu alipotafutwa, alifunguka: “Kweli nimesikia ishu
kama hiyo ila kinachonishangaza na kunisikitisha ni kwamba siku hiyo ya
tukio inayotajwa mimi nilikuwa nyumbani na siku nzima sikutoka kwenda
popote, hata hiyo Mbezi iliyotajwa mimi siielewi kabisa, hata lile gari
mimi sina gari la aina hiyo wala sijawahi hata kulipanda gari hilo na
huyo Young Dee nina muda mrefu sana sijaonana naye,”
“Usiku wa kuamkia leo nilimpigia mtangazaji mmoja ambaye aliirusha
habari hiyo redioni, nikataka kujua ameipata wapi habari hiyo? Akanijibu
kwamba amepata tetesi tu. Sasa kama ni tetesi kwa nini asichunguze
kabla hajanichafulia jina?”
“Pia alisema kuna askari wa doria walitukamata, nikamtaka anipeleke
hicho kituo cha polisi tulikopelekwa ili tuthibitishe kama ni kweli
maana ishu hii inanichafua mimi na familia yangu, akashindwa kufanya
hivyo.
Source: Global Publisher.