Wiki iliyopita, wanamuziki wa Kigoma Allstars akiwemo Diamond
Platnumz na wengine walikuwa mjini Mombasa, Kenya kwenye show ya sehemu
ya ziara yao katika nchini za Afrika Mashariki. Pamoja na kupiga show
kali, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kenya, Recho aliwatia aibu
kubwa wasanii wenzie wakati wakiongea na waandishi wa habari baada ya
show.
"Mwanamuziki wa Tanzania aliwashangaza waandishi wa habari pale alipoongea mbele ya camera kuwa alihitaji kuridhishwa kimapenzi,"mtandao wa Standard Digital News, SDE umeandika.
"Recho, aliyekuwa akiongea na waandishi wa habari baada ya show mjini Mombasa, alisema alihitaji mwanaume wa kulala naye usiku huo. Akifedheheshwa kwamba hitaji lake halikufaniwa, muimbaji huyo maarufu kwa wimbo wake Upepo, aliwaponda waandishi na watu wengine waliokuwepo pale kuwa hawakuweza kum’handle’ mwanamke,"uliandika.
Mtandao huo uliongeza: Recho hakuwa msanii pekee aliyefedheheshwa usiku huo kwani mwenzake Maunda alionekana backstage akilia baada ya kuzomewa atoke jukwaani na umati.