Akizungumza
na gpl hivi karibuni nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar, msanii
huyo ambaye alibadili dini kutoka ukristo na kuwa muislam baada ya
kuolewa na mumewe, Sunday Demonte alisema anajisikia kurudi kwenye
ukristo kwa madai ya kumtumikia Mungu kikamilifu.
Akionesha
msisitizo katika hilo, Aunt alisema moyo wake umekuwa ukitamani
kusikiliza mafundisho na mahubiri ya kikristo pamoja na kusikiliza
nyimbo mbalimbali za injili.
Wakizungumzia
mawazo ya kuokoka ya msanii huyo, baadhi ya mashabiki wake walimshangaa
huku wakionesha wasiwasi wake juu ya kusilimu na kudai huenda kubadili
kwake dini ilikuwa danganya toto.
“Huyu
si aseme tu uislam umemshinda? Kasilimu juzijuzi tu hapa na kudai
ameanza kusali msikitini, leo anatuambia anatamani kuokoka, hawa mastaa
wetu wanamchezea sana Mungu,” alisema Rahma wa Kinondoni jijini Dar.
-gpl
-gpl