Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

Saturday, December 28, 2013

SIMULIZI ; Kosa langu ni nini.......part 1


WWW.KENNED1.WEN.RU
Ilikuwa ni siku ya jumannemida ya saa kumi na mbili jioniMzee Ndesanjo alikuwaakiendesha gari aina yaEskudo. Alifika nyumbani naharaka alishuka ndani ya garikitendo cha kuingia ndani tualianza kuita kwa sauti "MamaJoyce Mama Joyce" hukochumbani Mama Joyce alimsikiana kuitika "Abeeee Mumewangu,vipi mbona mbiyombiyo hivyo "? Alihoji MamaJocye huku akiwaanamuangalia mume wake kwaumakini. Mzee Ndesanjo ambaye nimume wa Mama Joyce,alionekana kuwa na wasiwasimwingi huku akimsisitiza mkewake ajiandae haraka "Hakunamuda wa kupoteza, "Mimindani siingii nenda kajiandaetunasafari ya kwendaMorogoro, kuna matatizoyamejitokeza. Rafiki yanguMzee Simba ambaye tunafanyakazi ofisi moja amefiwa namke wake wake inabidi tuwahikwenda msibani”Mama Joyce alinyamaza kimyakidogo kana kwamba kuna kituanatafakari kwani ile habariilimshtua "Mmmh jamani ni ninitena kilimfika kwani alikuwaanaumwa! masikini" Aliongeakwa masikitiko "Alikuwaanaumwa na ameugua kwamuda mfupi sana,wewe nendakajiandae tuondoke". MamaJoyce akamjibu "Lakini mumewangu watoto tutawaacha nanani"? Aliuliza Mama Joyce.Wakati huo Jocye na mdogowake aliyeitwa Jameswalikuwa wameenda shule ,Joyce alikuwa darasa la tano naJames akiwa darasa la kwanza.Na pale walipokuwa wakiishiilikuwa ni nyumba ya kupangaMaeneo ya Kimara Stop Overjijini Dar es salaam. Baba Joycealimgeukia tena mke wake"Hawa watoto tutamkabidhijirani yetu Mzee Ngonyani namkewe, kwani hatuendi kukaazaidi ya siku mbili wewejiandae tuondoke wakirudikutoka shule watakutamaagizo kutoka kwa mke waNgonyani".Baba Joyce aliongeakwa msisitizo.Kwa haraka Mama Joyceakaenda kwenye chumba chaMke wa Ngonyani nakumwachia maagizo yakuwaangalia watoto wake kwamuda wa siku mbili. Baada yahapo aliingia chumbani nakujiandaa tayari kwa safari,ambapo safari ilianza taratibuna baadaye Baba Joycealionekana kuendesha gari kwamwendo wa kasi “Mumewangu mbona unaendeshakwa kasi hivyo jamani punguzamwendo kidogo” Aliongeakwa kuonyesha hali ya uoga. Baba Joyce alicheka kidogo nakusema “Acha kuogopa Mkewangu mbona naendeshakatika mwendo wa kawaidasana”. Safari iliendelea wakiwanjiani maeneo ya Kidatu,ghafla gari lilipata pancha tairiya mbele na kupinduka.Ilikuwa ni ajali mbaya sanakwani Baba Joyce alifarikipalepale na Mama Jocyealikuwa ameumia sana sehemuza kichwani hivyo wasamariawema walimchukua nakumkimbiza hospitalini.Baada ya wasamariakumkimbiza hospitalini MamaJoyce ambaye kwa wakati huoalikuwa hajitambui, AskariPolisi walifika eneo la tukio nakuuchukua mwili wamarehemu wa Baba Joyce nakuupeleka chumba cha maitihospitali ya Morogoro. Garililikuwa limeharibika sanakutokana na ajali ilivyokuwambaya hivyo ulifanykautaratibu wa kulisogeza hadikituo cha polisi, wakiwahospitalini Mama Joyce alikuwahajitambui kabisa.Polisi waliamua kufanyautaratibu wa kufahamu nduguambao wangeweza kuwa nayekaribu kwa wakati huo, mmojawa wale Askari Polisialimwambia mwenzake "Sasatutafanyaje kuwapata nduguzao kwani huyu mamahajitambui na mume wakeamekwisha fariki inabidituwatafute ili waendelee nataratibu nyingine". Mwenzakeambaye alikuwa naye akamjibuna kusema "Inabidi tuangalienamba zilizopo katika simu zaoili tuweze kuwasiliana nandugu zao".........nini kitaendelea usikosesura ya .....2........ NI SIMULIZI YAKUSISIMUA AMBAYO KITABUCHAKE KIPO JIKONI. Niliwahikuiweka kidogo zamani sanalakini hii ya sasa imekamilika namarekebisho yamefanyika kwaumakini. Endelea kupatauhondo.

Please Give Us Your 1 Minute In Sharing This Post!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com