MACHAFUKO
yanayoendelea ndani ya Baraza la Mawaziri, ni wazi yanawaweka
waheshimiwa wengi katika wakati mgumu ambapo Jumapili iliyopita,
paparazi alimnasa mmoja wa mawaziri (jina tunalo), kwenye nyumba ya
sangoma aliyefahamika kwa jina moja la Bwehe, Kijiji cha Mlingotini, Bagamoyo, Pwani.
Habari
zinadai waziri huyo alikwenda kwa Bwehe ili kufanyiwa madongoloji
(nguvu za giza), lengo kuu likiwa kuimarisha nyota yake ili Rais Jakaya
Kikwete atakapofanya panguapangua, jina lake liendelee kutamalaki.
Awali,
Jumamosi iliyopita paparazi wetu alipokea simu kutoka kwa msomaji wetu
aliyesema: “ fikeni Mlingotini kesho asubuhi mtamuona mheshimiwa …
(anataja jina la waziri) kwa mganga wa kienyeji.”
Timu
ya mapaparazi wetu ilianza safari alfajiri ya Jumapili iliyopita na
ilipotimia saa 12:50, tayari ilikuwa imekwishawasili Mlingotini na
kupiga kambi jirani na kwa Bwehe.
Hata
hivyo, ugunduzi wa waandishi wetu ni kwamba wengi waliosema
hawakumuona, ni dhahiri hawamjui, kwa hiyo haikuwa rahisi kupata taarifa
zake.
Saa 3:35 asubuhi, waziri huyo alikuwa hajawasili, hivyo kuanza kuzitilia shaka taarifa za mtoa habari.
Timu
ya mapaparazi, ilituma taarifa makao makuu kwamba taarifa za waziri
huyo inaonekana ni feki lakini muongozo wa kuendelea kusubiri
ulifanikisha jawabu ilipotimia 3:54, pale gari aina ya Nissan X-trail
lilipowasili nyumbani kwa sangoma huyo.
Kilichotendeka
ndani hakikuweza kujulikana lakini waziri huyo alitumia takriban saa 4,
kwani saa 8:07 mchana alitoka, akaingia kwenye gari na kutoweka.
Jitihada
za waandishi wetu kumuwahi ili kumuhoji sababu ya kwenda kwa sangoma
ilishindikana maana alipiga hatua kama za umeme kutoka ndani, kuingia
kwenye gari, kuwasha na kuondoka.'
Mwandishi
wetu alipomtafuta waziri huyo kwa simu, alipopatikana na kuulizwa ni
kwa nini alikwenda kwa sangoma, alinyamaza kwa sekunde kadhaa kisha
akazima simu.
Bwehe alipoulizwa na mwandishi kuhusu mgeni wake ambaye ni waziri, alikuwa mkali, akasema: “Mnataka kuingilia kazi yangu? Mnataka kujua nguvu nilizonazo? Endeleeni kunifuatilia na mtaniona.”
Habari
zinasema kuwa tangu machafuko katika Baraza la Mawaziri yatokee, hali
imekuwa tete na wengi wao wanaoamini nguvu za giza wamekuwa
wakijielekeza kwa waganga wa kienyeji kwa imani kwamba huko ndipo
watapata nusura.
Imebainishwa
kuwa wimbi la mawaziri kwenda kwa waganga, lilianza tangu Katibu Mkuu
wa CCM, Abrahman Kinana, alipozindua kampeni inayoitwa ‘safisha mawaziri
mizigo’, hivyo wengi wao kukimbilia kwa sangoma kwa imani kwamba
watawezeshwa kukaa upande salama.
Bila
shaka, machafuko ya Ijumaa iliyopita bungeni, yaliyofuata baada ya
kusomwa kwa ripoti ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, iliyoelezea
athari za Operesheni Tokomeza Ujangili (Otu), yanachagiza wenye imani
dhaifu kujikita kwa waganga wakiwaona ni wakombozi wao.
Ripoti
hiyo, ilisababisha mawaziri wanne, Dk. Hamis Kagasheki (Maliasili na
Utalii), Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi
na Jeshi la Kujenga Taifa) na Mathayo David (Uvuvi na Maendeleo ya
Mifugo) kung’oka, huku Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika kikaango
kikali.
Habari
zinasema kuwa wakuu wa mikoa kwa nafasi zao za kuwa wenyeviti wa kamati
za ulinzi na usalama kwenye maeneo yao, wapo kwenye tetemeko kwa sababu
unyama waliofanyiwa wananchi, nao hawawezi kupona kwa sababu kama
wangewajibika ipasavyo, ukatili uliotendeka usingefanyika.
-GPL