VIDEO
Queen, Agnes Jerald ‘Masogange’ hivi karibuni alibambwa maeneo ya Sinza
Kamanyola jijini Dar akijiachia na anayetajwa kuwa ni mpenzi wa Jack
Patrick, Juma Khalid ‘Jux’.
Wawili
hao walibambwa kwenye duka moja lililopo maeneo hayo baada ya Jux kutua
kutoka China huku Agnes akionekana kama anayemfariji kwa tukio la Jack
kunaswa na madawa ya kulevya.

Akiuzungumzia
ukaribu wake na Jux, Masogange alisema: “Wala hakuna lolote kati yangu
na yeye. Mimi na wale akina Jux pamoja na dada yake ni watu wangu wa
karibu sana tunaojuana muda mrefu hivyo tulikuwa tunabadilishana mawazo
tu.”
Jux
na Jack wamekuwa wakionekana katika mitaa ya China wakila bata huku
kukiwa na madai kuwa ni wapenzi na kuonekana kwa Jux na Masogange
wakijiachia kumeibua maswali mengi.
-GPL